STAA anayefanya
vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa
anatamani aone mastaa wawili ambao wana bifu kali, Wema Sepetu na Kajala
Masanja wanamaliza tofauti zao kwani maisha ni mafupi.
Akizungumza na gazeti hili, Aunt alisema kati ya mabifu ambayo angependa
yaishe ni la Wema na Kajala kwani wapo wasanii wamefariki dunia wakiwa
na bifu huku wale waliobaki ambao walikuwa na mabifu nao wakitamani
waamke walau mara moja wamalize tofauti zao lakini haikuwezekana.
“Jamani
maisha haya ni mafupi sana na tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wenzetu
tuliokuwa nao lakini sasa hivi hawapo tena, natamani sana Wema na Kajala
wamalize tofauti zao kwani ipo siku watakuja kujuta siku ambayo mmoja
wao atakapokuwa hayupo japo siwaombei ila hilo ndilo tamanio langu
kuwaona wakizungumza,” alisema Aunt.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Chapisha Maoni