Rehema Chalamila 'Ray C'.
STAA wa
Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ambaye anatumia dozi ya
kumwezesha kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, amesema kuwa mama yake
mzazi yu mgonjwa sana, akisumbuliwa na maumivu makali, Ijumaa Wikienda
lina mkasa kamili.
Mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, staa huyo
alisema kwa zaidi ya siku tatu mfululizo, mama yake alishindwa kupata
usingizi kutokana na maumivu ya mifupa ya miguu yaliyomfanya avimbe
miguu, kitendo kilichosababisha ajikute akilia kama mtoto mdogo.
“Ujue mara ya kwanza aliuguaga na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
baadaye Mungu alimjalia akapona lakini naona ugonjwa wake umerudi tena.
Anasumbuliwa na mifupa ambayo inamfanya wakati mwingine avimbe miguu
hadi anashindwa kutembea,” alisema nyota huyo maarufu kama Kiuno Bila
Mfupa.
Alisema mama yake amekuwa akipata shida kutembea kiasi kwamba Ijumaa
iliyopita, alimpeleka hospitali ya Wachina iliyopo Sinza ili kupata
vipimo na dawa, lakini haikusaidia.
“Hapa ninapoongea na wewe leo Jumamosi Machi 14, nipo kwenye Hospitali
ya Misheni hapa Tegeta tumekuja kupata matibabu na kalazwa kwa muda ili
afanyiwe vipimo vya MRI, maana leo usiku hajalala kabisa kwani muda wote
alikuwa akilalamika tu miguu inamuuma.
“Imefikia wakati hadi nahisi maumivu yake na nabaki nalia tu, nampenda
sana mama yangu kiasi kwamba natamani hata ningekuwa na fedha za kutosha
kama zamani, hivi sasa ningekuwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi,
anateseka usiku na mchana,” alisema Ray C.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Chapisha Maoni